Ifanye akaunti yako ya YouTube ikuingizie pesa

Ifanye akaunti yako ya YouTube ikuingizie pesa


Kwa wale ambao wameshajua kuwa kuwa Youtube inaweza ikawa chanzo kikubwa tu ya mapato yako basi wapo huko na kila sekunde hela zinaingia kwenye akaunti zao.

Unaweza kuwa na akaunti kwenye YouTube lakini je, ni ya kibiashara au akaunti ya kawaida tu ambayo ni mara chache sana unaweka huko picha jongefu ili na wengine wameze kuona picha hiyo ya mnato? BOFYA HAPA kujua namna ya kuwa na akaunti ya kibiashara kwenye Youtube.

Igueuze akaunti yako kwenye Youtube iwe ya kibiashara zaidi.

Ukiwa tayari umeshafanikiwa kuwa na akaunti kwenye Youtube (ya kibiashara) na tayari ina video kadhaa au nyingi zinazovutia bila kusahau zinapata idadi ya watazamaji wanaoongezeka siku baada ya siku sasa unatakiwa ufikirie iwe chanzo cha mapato yako siku yoyote, saa yoyote na popote pale kwa kufuata hatua hizi:
Picha jongefu (video) kuwa chanzo cha pesa: Msingi wa kutengeneza pesa kupitia chaneli yako ya Youtube unaanzia hapa; bofya kwenye My channel>>>Video Manager>>>Enable monettization>>>Enable.
akaunti yako ya YouTube
Ukisharuhusu huu mpangilio basi hapo ndio itakuwa mwazo wa kujitengenezea kipato kupitia Youtube.
Vigezo. Kipengele hiki kinaweza kuonekana ni kigumu lakini kama picha jongefu zinakuwa zinaangaliwa kwa wingi basi utakuwa sehemu nzuri; ni lazima video ziwe zimeangaliwa angalau kwa saa elfu nne (4000) na uwe na watu wasiopungua 1,000 ambao watapata taarifa fupi mara tu utakapokuwa umepakia video kwenye chaneli yako ya Youtube.
Matangazo (Adsense). Unapoangalia picha jongefu halafu chini yake kuna tangazo dogo linalokuja na kupotea baada ya muda fulani lina maana yake na haliwezi tu kutokea tu. Unatakiwa kutengeneza akaunti kwenye Google AdSense>>>BOFYA HAPA.
Kwa kila mtu atakayebonyeza tangazo lile basi sehemu ya mapato ya lile tangazo yataingia kwenye akaunti yako kupitia PayPal hivyo ni lazima kuwa na akaunti ya PayPal. Pia kama mtu akatazama lile tangazo kwa sekunde chache utapata mgao wako.
Fuatilia mambo yanavyokwenda. Usiweke picha jongefu kwenye chaneli yako halafu ukasahau kutaka kujua kama inaangalia na wengi au la! Hapa unaweza kufanya makadirio ya kile ambacho unategemea kupata. Ndani ya kipengele cha My Channel bofya kipengele cha Analytics kuona mambo kinagaubaga.
akaunti yako ya YouTube
Ni muhimu sana kufuatilia mwenendo wa kile ulichokiweka kwenye chaneli yako ya Youtube.
Sambaza kwa wengine. Moja ya njia ya kuongeza kile ambacho unapata kwenye Youtube ni pamoja na kuwashikirikisha wengine ili waone video yako; unaweza ukaisambaza kwenye mitandao ya kijamii, tovuti, watu, n.k lengo likiwa ni kuongeza watazamaji/dakika za jumla zilizotazamwa.
Ukisambaza video yako kwa wingi na ikaangaliwa maana yake ni pesa itakayopata itaongezeka.
Kuwa mshirika na Youtube. Ni muhimu kuwa mshirika wa Youtube lakini tabidi uwe na jumla ya watu wasiopungua 15 elfu walioangalia picha mnato ulizoziweka kwenye chaneli yako kwa kipindi cha miezi mitatu tangu uanze kutumia chaneli yako kama chanzo cha pesa.

Anayekuwa mshirika wa Youtube anakuwa na uwanja mpana kutumia chaneki yake na hata kushinda zawadi kutoka Youtube kutokana na idadi ya watazamaji aliofikisha.

akaunti yako ya YouTube
Utabofya “Enable” kwenye ule ukurasa wa “Monetization”.
Tengeneza maswali/Ombi ushauri kwa wanaofuatilia chaneli yako. Kupitia Supp.me utatengeneza maswali/kutaka kupata mrejesho kutokana na video za kwenye chaneli yako kisha utatuma kwa wale wanafuatilia chaneli yako na wakijibu maswali yako kwenye Supp.me utapata mchao wako kutoka huko (Supp.me).
akaunti yako ya YouTube
Shirikisha watu wengi wameze kuona ulichokiandaa kwenye Supp.me ili uongeze kipato chako kwenye Youtube.

Hitimisho na kitu cha kukumbuka si lazima mpaka uwe umefanikisha kuweka video yote kwenye Youtube ndio uweze kuanza kuvuna pesa; bofya kwenye Monetization>>>Monetize with Ads. Kazi kwako sasa.

Chanzo: WikiHow
Reactions

Post a Comment

0 Comments