Kampuni ya mikopo mtandao ya TALA yafunga shughuli zake Tanzania

Kampuni ya mikopo mtandao ya TALA yafunga shughuli zake Tanzania


Kampuni ya TALA inayokopesha kwa njia ya mtandao wa simu za mkononi, imetangaza kufunga shughuli zake Tanzania.

Imetoa taarifa hiyo Jumanne Septemba 17, 2019 na kubainisha kuwa maelezo ya kina kuhusu uamuzi huo yatatolewa hivi karibuni.

Kampuni hiyo inayoendeshwa na teknolojia ambayo kwa sasa inafanya kazi nchini Kenya, Mexico,
India na Ufilipino hutoa mikopo ya haraka, na binafsi kwa wakopaji na kuvutia zaidi ya watu milioni 27 duniani.
tala tanzania
Tunasikitika kukutaarifu ya kwamba Tala kwa sasa haitatoa mikopo Tanzania. Tunashukuru kwa kutupa nafasi ya kukuhudumia na kuwatakia wateja wetu mafanikio.Wateja ambao bado wanadaiwa wanaweza kulipa mikopo yao. Tumia Tigo-Pesa lipa namba 888000 and nambari ya simu uliojisajilia na Tala kama akaunti yako,” inasomeka taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo.

Ripoti ya kampuni hiyo mwaka 2018 inaonyesha kuwa katika nchi za Afrika Mashariki asilimia 78 ya mikopo hutumiwa kwa biashara, asilimia 32 ya wateja wake wakiwa wanawake na wanaume, kati yao asilimia 68 wana umri chini ya miaka 34.

Reactions

Post a Comment

0 Comments