Kompyuta inaanza kuwa nzito kiufanisi.. Sababu ni nini?

Kompyuta inaanza kuwa nzito kiufanisi.. Sababu ni nini?



Unaweza ukawa umeshawahi kujiuliza swali hili; Kwa nini kompyuta inaanza kuwa nzito au kutofanya kazi vizuri baada ya muda?

Umenunua kompyuta umeitumia vizuri ila baada ya muda flani; miezi au ata miaka inaanza kuwa nzito na programu hazifanyi kazi vizuri tena kama awali. Unasasisha (update/upgrade) programu hizo na programu endeshaji (OS) lakini bado, kompyuta imekuwa nzito kwenye utendaji.

Je, ni nini kinasababisha?

> ‘Fragmented Data’ – Mgawanyiko wa Data.

Hii inamaanisha mpangilio usio sahihi wa data katika diski (HDD/SSD). Mpangilio huo usio mzuri husababishwa na hatua nyingi za kuingiza na kutoa programu mbalimbali. Pale zoezi la kupakia (install), kusasisha (update) au kufuta (uninstall) linafanyika diski inakuwa inajitahidi kuzipanga data zako katika mpangilio rahisi kwa ajili ya data hizo kuweza kusomeka.
Kwenye diski si kwamba data ya programu moja inakuwa kwenye sehemu/upande fulani tu wa diski, data zinasambazwa maeneo mbalimbali. Kama unatumia diski ya HDD basi ndio zinaathirika zaidi katika usomaji wa data ambazo zimekuwa fragmented/kusambazwa maeneo mbalimbali ya diski, athari yake huwa ni upunguaji wa kasi/uharaka katika ufanisi. Ila kwa diski za SSD ufanisi wake huwa hauathiriki sana na suala hili.
Jinsi ya kutatua; Defragmenting: Kwenye eneo la settings/mpangilio wa diski kuna eneo la wewe kuchagua kuifanya diski yako ifanye mpangilio mzuri wa data kila baada ya muda. Angalizo!-Tumia uwezo huu kwa diski za HDD tuu, kwa diski za SSD inaweza sababisha kua data zako zote na diski yenyewe.

> Toleo la programu endeshaji (OS)

Kabla hujasasisha (upgrade) kompyuta yako kwenye toleo jipya la programu endeshaji (OS) ni vizuri kusoma sifa za kompyuta ambayo toleo la programu endeshaji hili litafanya kazi kwa ufanisi bora zaidi.
windows 10
Kila matoleo mapya ya programu endeshaji yanavyozidi kutolewa ndivyo ambavyo yanakuwa yanahitaji kompyuta zenye uwezo mkubwa zaidi. Utumiaji wa matoleo ya kisasa sana ya programu endeshaji bila wewe kufanya maboresho ya baadhi ya vipuri muhimu vya kompyuta yako kama vile RAM vinaweza kuathiri utendaji kazi wa kompyuta hiyo.

> Uchafu wa kompyuta: Usafi wa vifaa na wa kiprogramu endeshaji

Ili kompyuta ifanye kazi vizuri sehemu zake za ndani kama vile CPU, RAM, uso wa juu, n.k vinatakiwa viwe katika hali ya usafi ili kuisaidia kuondoa joto linalosababishwa na ufanyaji kazi wake. Kama maeneo ya ndani ya kompyuta yatakuwa hayasafishwi mara kwa mara basi patajaa vumbi, n.k na hivyo kuifanya kompyuta kushindwa kufanya kwa ufanisi. Hapa ndio saa inaweza hata kusababisha kompyuta kujizima zima na matatizo mengine kama hayo.
Uchafu wa kiprogramu unasababishwa na uwepo wa masalio ya data ambazo hazitumiki kwenye diski, data hizo zinakuwa kama masalio ya hatua mbalimbali za upakuaji programu mbalimbali pamoja na masasisho yake (updates). Pia uchafu mwingine ni uwepo wa programu ambazo hazina ulazima kuwepo au hauzitumii nazo zinakuwa zinafanya kazi ndani kwa ndani bila wewe kujua (background processes), cha msingi ni kuhakikisha mara kwa mara unaangalia programu ambazo zipo kwenye kompyuta yako na kuondoa zozote ambazo hauzihitaji.

Sasa unafahamu kwa nini kompyuta inaanza kuwa nzito kiufanisi, soma makala mengine kufahamu cha kufanya – Kwa haraka haraka ufanye nini kuboresha ufanisi wa kompyuta au laptop yako?

Reactions

Post a Comment

0 Comments