Mambo yote yaliyotangazwa na Apple Septemba 2019! #iPhone11 #AppleTV

Mambo yote yaliyotangazwa na Apple Septemba 2019! #iPhone11 #AppleTV



Kwa Apple tarehe 10 Septemba 2019 ilikuwa ni siku ya kutambulisha simu zao mpya – iPhone 11, ila sehemu kubwa ya utambulisho huo ulihusisha zaidi huduma zake zingine mbalimbali.

Apple septemba 2019 iphone mpya
Apple Septemba 2019: Utambulisho wa iPhone 11
iphone 11
iPhone 11 Pro Max: Muonekano
Katika tukio hilo lilifanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo Cupertino, Apple walitambulisha kwa undani huduma zao za Apple TV, iPad, iPhone 11, mfumo wa magemu wa Apple Arcade, na saa mpya ya Apple Watch Series 3.

Saa ya Apple Watch Series 3

Wametambulisha toleo jipya la saa ya Apple Watch Series 3. Kikubwa hapa ni kwamba saa hizo zimepunguzwa bei kutoka dola 279 (zaidi ya Tsh 600,000/=) na sasa toleo hili jipya litapatikana kwa dola 200 tuu (takribani Tsh 430,000/=)

Huduma ya Apple TV+

Huduma ya kutazama vipindi kwa mfumo wa mtandao, mpinzani wa huduma ya Netflix, Apple TV+ itaanza kupatikana Novemba na itagharimu dola 4.99 kwa mwezi (Takribani Tsh 11,000/=)

iPad mpya ni takribani Tsh 700,000

Pia Apple wametambulisha iPad mpya ya ukubwa wa display wa inchi 10.2. Wameongezea uwezo mzuri wa iPad kutambua na ufanyaji kazi wa keyboard za Bluetooth. Pia kuna utumiaji wa kalamu spesheli unaweza kutumika hasa hasa kwa kwa matumizi ya uchoraji n.k. iPad mpya inaanza kwa bei ya dola 329 za Kimarekani.

Apple Arcade

Apple wamekuja pia na huduma na mfumo wa magemu unaotambulika kama Arcade. Kupitia malipo ya dola 5 kwa mwezi (Takribani Tsh 11,000/=) mtumiaji ataweza kucheza magemu ya aina mbalimbali bure kwenye iPhone au iPad. Hadi sasa Apple wamesema mfumo huo una magemu zaidi ya 100.

iPhone 11.

iphone 11
iPhone 11: Zinakuja katika rangi mbalimbali
Kama utakuwa umegundua kwa sasa moja ya vita kubwa kiushindani katika simu janja ni eneo la kamera. Simu ya iPhone 11 inakuja na mfumo unaotumia kamera mbili zote zikiwa ni za megapixel 12 kila moja. Kamera hizi kwa pamoja zinahakikisha picha zinakuwa katika ubora mzuri ata kama ni picha ambazo zinahusisha sehemu pana sana (wide & ultra-wide).
Ata kamera ya selfi pia ni ya pixel 12 ila kwa mara ya kwanza kwa iPhone utaweza kurekodi video za 4K kwenye kamera ya selfi.  Simu hii itaanza kupatikana kwa bei ya dola $699 (Takribani Tsh 1,600,000/=).

iPhone 11 Pro na iPhone 11 Pro Max

iphone 11 pro apple septemba
Tofauti kubwa iliyokuja katika simu za iPhone 11 na ata hizi za iPhone 11 Pro ni sehemu ya kamera. Kuna waliopenda na ambao hawajapendezwa na muonekano huu.
Ukiacha toleo la iPhone 11, kuna matoleo mengine mawili mengine..nayo ni iPhone 11 Pro na iPhone 11 Pro Max. Simu hizi mbili ni simu ambazo wamezipa uwezo mkubwa sana wa kiutendaji kiasi ya kwamba Apple wanaamini zina nguvu/uwezo mkubwa kiutendaji kuliko ata laptop nyingi zinazopatikana sokoni kwa sasa. Hii ni kutokana na utumiaji wa chip/prosesa yao mpya kabisa ya A13, pia nje ya zile kamera mbili kama kwenye toleo la iPhone 11, hizi simu mbili zinakuja na kamera ya tatu inayozidi kuongeza ubora wa picha zake (telephoto lens).
iPhone 11 Pro 11 apple septemba
iPhone 11 Pro: Muonekano
Display ya simu hizi ni ya kiwango cha juu ya 4K – teknolojia na kiwango walichokipa jina la Super Retina OLED. iPhone 11 Pro ikiwa na display ya inchi 5.8 wakati iPhone 11 Pro Max ikiwa na display ya inchi 6.5.
Bei: iPhone 11 Pro inaanzisha dola $999 (Takribani Tsh 2,300,000/=) wakati iPhone 11 Pro Max inaanzisha dola $1099 (Tsh 2,530,000/=).
Simu za iPhone 11 mpya zitaanza kupatikana tarehe 20 mwezi huu (Septemba).

Je una mtazamo gani juu ya simu hizi mpya kutoka Apple pamoja na huduma zao mbalimbali mpya za kulipia?

Reactions

Post a Comment

0 Comments