Namna ya kuandika ujumbe haraka kwenye Gmail

Namna ya kuandika ujumbe haraka kwenye Gmail



Katika dunia ya leo njia mojawapo ya kufanya mawasiliano ni kupitia barua pepe na kama ni mtu ambae unatuma jumbe kupitia Gmail ni vyema ukafahamu namna ya kuandika ujumbe haraka.


Kwenye simu zetu tunapoandika ujumbe mfupi wa maneno yale maneno ambayo herufi zake za mwanzo zinafanana na neno la Kiingereza huwa linamalizika kujiandika pasipo wewe kutarajia na usipokuwa makini kuhakiki kile ulichokiandika kwenda kwa mlengwa kutakuwa na uwezekano wa ujumbe wako kutoeleweka.
Kwenye Gmail kitu hicho kipo na kwa maoni yangu kinasaidia sana hasa kama wewe ni mtu ambae unafanya mawasiliano yako kupitia barua pepe kwa lugha ya Kiingereza lakini utofauti wake na kwenye simu ni lile neno ambalo linatokea halitaungana na mengine pasipo wewe mwandishi kuruhusu.
Video Player
00:00
00:40

Jinsi ya kupangilia kuweza kuandika ujumbe haraka kwenye Gmail.

Vitu vyote vinaanzia kwenye mpangilio (settings) ambapo ni lazima uruhusu ili kila utakapokuwa unaandika ujumbe kupitia barua pepe uwe unatumia muda mfupi kumaliza. Unachotakiwa ni kungia Settings>>General>>Smart Compose kisha ruhusu kwa kuchagua “Writing suggestions on.
kuandika ujumbe haraka
Jinsi ya kuweka mambo sawa ili kuweza kuandika ujukwa haraka kwenye barua pepe.

Ukishaweka kila kitu sawa na ukiingia kwenye sehemu ya kuandika ujumbe kupitia barua pepe mathalani ukaandika “How” na maneno mengine yakatokea “are you?” kukubali utabonyeza mshale unaonyesha kwenda kulia kwenye kicharazio na neno zima “How are you?” litatokea.

Anza sasa kuandika jumbe kwenye barua pepe kwa kutumia mbinu hiyo iliyoelezwa hapo juu. Teknolojia ni yetu sote, usisite kushirikisha na wengine.

Reactions

Post a Comment

0 Comments