Ufanye nini kuboresha ufanisi wa kompyuta au laptop yako?

Ufanye nini kuboresha ufanisi wa kompyuta au laptop yako?




Kuboresha ufanisi wa kompyuta au laptop yako ufanye nini? Hili ni swali tulilopokea kutoka kwa mmoja wa wasomaji wetu. Kuna mambo mengi yanayoweza yakawa yameathiri utendaji au ufanisi wa kompyuta au laptop yako.

Sababu mbalimbali tumezielezea kwenye makala yetu -> Kompyuta inaanza kuwa nzito kiufanisi.. Sababu ni nini?, hapa tunakuelezea jinsi ya hatua kadhaa chache za haraka unazoweza kuzichukua ili kusaidia kuongeza ufanisi wa kompyuta yako.

Laptop au kompyuta inayotunzwa kwa usafi itadumu sana kiufanisi na utaiepusha na uharibifu wa vifaa vya ndani.

> Isafishe mara kwa mara

Ondoa vumbi vumbi na uchafu mwingine wowote. Unaweza kutumia vifaa vya kupuliza upepo (Air Blower) kufikia na kuondoa vumbi la ndani sana ya kompyuta yako.

> Weka programu unazotumia tuu

Pakua programu (software) unazohitaji na kutumia tuu; Ondoa programu ambazo unafahamu huziitaji au kuzitumia kwenye kompyuta yako.

> Tumia toleo sahihi la programu endeshaji (OS)

Tumia programu endeshaji sahihi kwa sifa ya kompyuta yako. Je ni kompyuta ya miaka mingi sana? Basi fahamu toleo jipya zaidi la programu endeshaji halitaweza kufanya kazi kwa ufanisi mzuri. Kama ni kompyuta ya kisasa basi hakikisha unatumia programu endeshaji ya kisasa.
Baada ya miaka kadhaa futa kabisa kompyuta na ingiza programu endeshaji upya (OS). Mara zote ukisasisha programu endeshaji mara nyingi nayo inaathiri ufanisi ukilinganisha na mtu

> Ongeza RAM

RAM ni moja ya kifaa cha bei nafuu kwenye kompyuta ambacho kinaweza kuongeza ufanisi kwa kiasi flani kwenye kompyuta yako. Kompyuta yenye RAM ndogo (GB 2 n.k kulingana na mahitaji) inauwezo mdogo wa kuhimili ufanyaji kazi wa programu mbalimbali kwa wakati mmoja. Kulingana na aina ya kompyuta au laptop unaweza kupata RAM ya ukubwa mzuri tuu kuanzia Tsh 50,000 hadi Tsh 200,000.

> Badili diski ya Drive C – Kutoka diski ya HDD kwenda diski ya SSD

Diski za SSD zinatumia teknolojia ya kisasa zaidi katika usomaji na uandikaji data kwenye kompyuta na hivyo zinakasi kubwa zaidi na kuifanya programu endeshaji pia kuwa na ufanisi wa zaidi ya mara mbili kwa kompyuta yenye sifa zote zikifanana kasoro ikiwa ni moja kuwa na HDD na nyingine SSD kama diski C; ya programu endeshaji.

Je umejifunza kipya leo? Endelea kutembelea mtandao wa Teknokona na kuwasiliana nasi kupitia Twitter- > @hajimuron au Facebook @MuronTv.

Reactions

Post a Comment

0 Comments