Asilimia 40 Ya Watuamiaji Wa iPhone Watahama Kama Watapewa Bure Simu Ya Android! #Tafiti #iOsVsAndroid

Asilimia 40 Ya Watuamiaji Wa iPhone Watahama Kama Watapewa Bure Simu Ya Android! #Tafiti #iOsVsAndroid



Ukiachana na tafiti jaribu kujiuliza kitu kimoja hivi simu janja unayoitumia unaipenda kiasi gani? ikitokea mtu akaamua kukupa nyingine ambayo ni toleo la mbadala kabisa kawa mfano kutoka Android kwenda  iOS utakuwa tayari?

Ni tafiti ya haraka haraka ambayo imefanyika na Signs.com ni kwamba imegunduliaka watumiaji wengi sana wa Apple wana mapenzi ya dhati na vifaa vya kampuni hiyo. Ni wazi kuna watu pia ni wapenzi wa dhati wa Android na kuwahamisha  na kwenda katika vifaa vingine ni vigumu kabisa.
Tafiti hii haikuwa kubwa sana kwani lengo lake kubwa lilikuwa ni kutaka kujua tuu ni kiasi gani cha watu kinweza kuhama na kaunza kutumia kifaa — kompyuta au simu janja — kingine (cha kampuni lingine).
Katika kuliteka soko Windows inamiliki aslimia 88 ya kompyuta zote wakati Mac Os ikiwa inamiliki asilimia 9 tuu, umiliki huo ukiwa kama programu endeshaji katika kompyuta. Usishangae hilo tuu kingine ni kwamba Android nayo inachukua asilimia 72 ya soko ukilinganisha na iOS ambayo ni asilimia 28 ya soko.
Microsoft OS (Windows) VS Mac Os
Microsoft OS (Windows) VS Mac Os
Mtandao wa Sing.com umefanya tafiti kwa wakazi wa marekani wapatao elfu moja, Utafiti huu ulikua juu ya mapendelea kati ya Apple na Microsoft. Tafiti imeonyesha kuwa asilimia 35 tuu ya watumiaji wa Mac watahama kwenda katika Windows kama wakipewa PC za bure. Kingine cha kuvutia ni kwamba asilimia 49 wamekataa katu katu kuhama hata wakipewa kompyuta zingine
Asilimia 15 wameshindwa kuja na maamuzi ya kuhama au kubaki hivyo wamebaki katika lile kundi ambalo limeshindwa kufanya chaguzi. hii yote ilikua ni katika kompyuta lakini hivi umeshafikiria katika swala zima la simu janja, matokeo yatakuwa vipi?
Android VS iOS
Microsoft OS (Windows) VS Mac Os
Katika swali hilo hilo watumaiji wa simu waliulizwa kama wanaweza badilisha simu kama wakipewa nyingine bure na majibyu yalikuwa kama ifuatavyo. Asilimia 44 ya watumiaji wa iPhone walikataa katu katu kuhama kwenda katika kifaa kingine wakati asilimia 40 wakakubali kama wakipewa kifaa kingine bure.
Asilimia 51 ya watumiaji wa Android wameweka wazi kuwa wapo tayari kuhamia katika iPhone kama wangeipata bure, asilimia 34 tuu walisema wao hawawezi kuhama hata kwa dawa!

Jionee Tafiti Hiyo Katika Picha (Microsoft VS Mac, Android Vs iOS)

watumiaji wa iphone watahama Android Vs IOS, Microsoft VS Mac OS
Watumiaji wa iPhone Watahama wakipewa simu za Android, ila pia asilimia 51 wa Android pia wanasema watahama wakipewa simu nyingine ya bure
Chanzo: Sing.Com

Endelea kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwa Habari Kede Kede Zinazohusu Teknolojia Kwa Ujumla. Kumbuka Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Reactions

Post a Comment

0 Comments